Ukumbi ni moja ya jambo
muhimu na linapaswa kuzingatiwa baada ya kutengeneza nia ya kufanya
Harusi. Ingawa wahusika wanatakiwa kuwa
makini na kuhakikisha wanafanya utafiti wa aina ya ukumbi na eneo ukumbi ulipo.
Baada ya hapo wanafikisha taarifa ya ukumbi husika kwa wajumbe wa maandalizi ya
Harusi yenu.
Harusi Link inaweza kuwa
msaada wako. Angalia katika ukurasa wetu unaweza kupata ukumbi unaouhitaji.
Mambo yafuatayo yanaweza
kukusaidia katika kutimiza kwa usahihi jambo la kupata ukumbi.
·
Fikiri idadi ya wageni wako
·
Fikiria juu ya ukumbi na chagua kama kumbi Zaidi
ya mbili.
·
Fanya uchaguzi juu ya kumbi baada ya
kuzitembelea na kuziangalia
Wakati
unafanya uchaguzi wa ukumbi hakikisha pia unazingatia haya:-
i.
Juu ya Maegesho ya magari
ii.
Idadi ya Watu
iii.
Huduma ya Chakula (Je wanatoa hapo au
unaweza kuja nacho)
iv.
Huduma ya Vinywaji na Wahudumu(Je wanatoa huduma ya vinywaji na
wahudumu?). endapo utakuta wanatoa huduma hii, fikiria juu ya bajeti yake, kama
hawatoi fikiria juu ya mtu atakayekuletea vinjwaji. Usisahau kulipia malipo ya
awali ya Vinjwaji. Vipi kuhusu shampaigne (Fuata mapendekezo, kama je iwe ya
kilevi au la!)
v.
Viti na Meza vinapatikana hapo?
vi.
Muziki unapatikana hapo?
vii.
Keki je?
viii.
Vipi kuhusu mapambo na gharama zake.
*Zingatia kufanya booking
na Malipo tangulizi yenye stakabadhi halali.
“TUNAKUTAKIA MAANDALIZI
MEMA YA HARUSI”. +255 676 251912