Huduma
ya Video na Picha ni muhimu kwenye Harusi . Huduma hii inawezesha Maharusi
kupata kumbukumbu juu ya tukio Zima la harusi.
Ingawa
uchaguzi wa nani akupe huduma hii ni jambo ambalo linahitaji umakini. Ili
kurahisisha jambo hili unapaswa kuzingatia yafuatayo: -
·
Fikiria
juu ya aina ya picha na Video unazohitaji
·
Fikiria
juu ya bajeti yako katika swala hili
·
Fikiria
juu ya idadi ya picha unazohitaji
·
Tafuta
watoa huduma wasiopungua wane (Unaweza kuwapata kupitia Harusi Link)
·
Watembelee
ili kujua walipo na uone sample ya kazi zao
·
Chagua
mtoa huduma uliyeona anafaa. Katika uchaguzi hakikisha unatumia kigezo cha
ubora wa picha.
·
Baada
ya kufanya uchaguzi lipia kabisa malipo tangulizi (Advance)
·
Mpe
ratiba ya HARUSI Wiki moja kabla ya Harusi, hii itakusaidia sana kujua na yeye
kupanga ratiba yake vizuri.