Kabla/Before Harusi


Kabla ya Harusi unapaswa kuhakikisha kuwa umekaa na mwenzio na kuelewana juu ya nia yako ya kuamua kufunga ndoa au kufanya Harusi. Ni jambo jema sana  mkiamua kwa pamoja namna, aina na wapi Harusi hiyo itafanyika, Je Mtaifanyia ukumbini au nyumbani au itaishia tu kanisani au msikitini?.

Ila ni lazima kuzingatia haya kabla ya  Harusi unayoitarajia!

  • Fikiri endapo utafanya sherehe ya Kuvalishwa au kumvalisha Bi harusi mtarajiwa Pete. " Endapo utaamua kufanya tendo hilo, Panga siku ya tukio hilo kabisa na mfahamishe mwenza wako"
  •  Fikiri kwa pamoja kama je kutakuwa na Kichen Party au la?  Fanya maandalizi yake ili kuhakikisha kuwa Harusi yenu inafanikiwa.
  • Kuna wanaofanya Send Off, Je utafanya hivyo? Ni Swali la kujiuliza kabla ya Harusi na hili linafanyika kwanza kabla ya harusi yenyewe.
  • Fikiria kama je kutakuwa na tukio maalumu la kupiga picha maalumu. Andaa location, Kumbuka location au mahali pa kupigia picha panalipiwa kwa baadhi ya maeneo, hivyo fanya booking mapema na kama kuna malipo lipia kabisa.
  • Fikiria juu ya maandalizi ya Fungate

Mambo Mengine muhimu yakuzingatia na kufuata kabla na wakati unaandaa harusi yako!

   Andaa File la Kuhifadhi Taarifa za Harusi yako

Ni muhimu sana kuandaa jalada au File ambalo utalitumia kuweka kumbukumbu za maandalizi ya Harusi yako , ikiwemo Bajeti ya hausi, Taarifa za vikao, Stakabadhi /Receipts, Majina ya Wageni n.k

Aina ya Harusi

Fikiria kama je unataka harusi ya aina gani, Fikiria unataka harusi ya namna gani, ndogo au Kubwa , je itahusisha watu wa karibu tu au la, itakuwa ya kawaida au ya  kifahari, ya kati au la?. Endapo utazingatia hili itakusaidia sana kutimiza swala la Harusi.

Aina ya Ukumbi

Zingatia  na Kuwa makini juu ya hili, Fikiri kwa makini juu ya  je waalikwa watasherekea katika ukumbi wa nje? au wa  Ndani? . Na endapo utapata jibu la aina ya ukumbi , nenda fanya booking, ukiukuta upo wazi lipia malipo tangulizi ili uweze kujihakikishia kuwa harusi itafanyika kwa siku iliyopangwa.

Usafiri

Fikiria juu ya usafiri wa watu wanaotoka mbali. Hakikishwa mipango inakamilika kwa wakati?. Fanya Booking ya Hotel au Nyimba watakayoshukia wageni wako ili kuwahakikishia usalama na malazi katika sehemu tulivu.


Andaa siku yako ya Harusi

Hakikisha unaandaa siku yako ya harusi kabla ya kuwashirikisha watu unaotegemea kuwaalika. Kaa na Bi Harusi mtarajiwa mpange kwa pamoja siku na Mwaka kwa ajili ya Harusi yenu.

Hapa zingatia sana Utayari wa watu wenu wa Karibu (hasa katika swala la muda), Upatikanaji wa Ukumbi au Kanisa Fulani, Angalia kama ni siku ya sikukuu au la. Usisahau kuwahusisha familia juu ya hili.

Andaa siku ya kuanza Vikao na Alika wajumbe katika kikao chako

Hatua hii ni muhimu sana kwani , ni hatua ambayo inawafanya wajumbe walioalikwa wajisikie wao ni sehemu ya jambo hili na kwamba wanapaswa kulibeba. Katika vikao vyako hakikisha mambo yafuatayo yanatimizwa:-

·         Bajeti ya Harusi inatengenezwa na kuwasilishwa kwa wajumbe

·          Mc na Muziki vinapatikana

·         Watoa huduma zingine wanapatikana ( Pia kupitia mtandao huu watoa huduma wote utawapata kwa haraka)

·          Ratiba ya Harusi

·          Kamati mbalimbali zinaundwa ili kufanikisha Harusi

·           Wajumbe wafahamishwe  Rangi ya Harusi

Chagua Wasimamizi

Fikiria juu ya wasimamizi wa harusi yako, Wape taarifa na uwaeleze namna ya unavyofikiri juu ya harusi yako. Endapo wana mawazo ya kujenga, wape fursa ya wao kukushauri wanachofikiri ni sahihi.

Mavazi na Mambo mengine yanayoendana

Fikiri kama unaenda kununu mavazi au unatoa order ya kushonewa, au Unakodisha. Weka mda wa kutosha juu ya hili ili kupata chaguo la mavazi yaliyo sahihi.

Usiku wa Harusi

Hakikisha kuwa unapaki vitu vyako muhimu siku moja kabla ya Harusi. Kwa kufanya hivi itaufanya usiku wa Harusi yako uende sawia. Kama kuna vitu vinakosekana fanya mpango wa kununua.

Hakikisha unaweka vizuri vitambulisho vyako, pass ya kusafiria, au Kadi ya Mpiga kura . Hii itakusaidia endapo utafika kwenye hotel au sehemu uliyoiandaa kwa ajili ya kupumzika baada ya harusi na wakahitaji vitu hivyo.

Fungate

Kama utaenda fungate, fanya maandalizi kabisa, fanya booking ya Hotel au Sehemu maalumu kwa ajili hiyo,Hakikisha unajiandaa kifedha pia ili kuifanya siku hiyo kuwa ya kumbukumbu kwenu.
................................................................................................................................................
Karibu Harusi Link | Chang'ombe Mtaa wa Toroli, Dar es Salaam| +255 676 251912/+255 714 992972