Kadi Na Mwaliko


    Kadi na Mwaliko : Muhimu Kuzingatia
     Hakikisha unawapa wageni wako wote kadi ya Mwaliko wa Harusi yako. Hii inasaidia sana na inaondoa usumbufu kwa kamati iliyopewa jukumu la mapokezi. Inawapa fursa ya kuwatambua wageni wako kwa urahisi.
    Kabla ya Yote:-
    • Fikiria juu ya idadi ya  wageni wako na waorodheshe kwa majina,hakikisha majina ya familia zote mbili unayaorodhesha pia.
    •  Anza kuyaandaa maneno  unayotaka kuandika kwenye kadi za Mwaliko,
    • Nunua au tengeneza kadi za mwaliko, watoa huduma za kadi watakusaidia kutengeneza (wasiliana nao kupitia mtandao huu). 
    • Wafahamishe  Wageni wako kwa kutuma ujumbe;  kwa watu walioko katika orodha yako kuhusu siku yako ya harusi,
    • Unashauriwa kutengeneza na kuzituma kadi za mwaliko walau mwezi mmoja kabla ya harusi
    Andaa ratiba ya harusi na kuidurufu/Kuiprint,Unaweza  kuambatanisha na kadi za mwaliko. Pia kumbuka kuwapigia simu kuwapa taarifa juu ya kukamilika kwa kadi za mwaliko wa harusi .
    KWA MAHITAJI YA KADI ZA HARUSI: +255 676 251912